10 Mimi niliongea na manabii;ni mimi niliyewapa maono mengi,na kwa njia yao natangaza mpango wangu.
11 Huko Gileadi ni mahali pa dhambi;huko Gilgali walitambika fahali,kwa hiyo madhabahu zao zitakuwa marundo ya mawe kwenye mitaro shambani.”
12 Yakobo alikimbia nchi ya Aramuakiwa huko alifanya kazi apate mke,akachunga kondoo ili apate mke.
13 Kwa nabii Mwenyezi-Mungu aliwatoa Waisraeli nchini Misri,na kwa nabii Mungu aliwahifadhi.
14 Waefraimu wamemchukiza Mwenyezi-Mungu sana.Lakini Mwenyezi-Mungu atawalipiza makosa yao,atawaadhibu kwa mambo maovu waliyotenda.