4 Yakobo akiwa bado tumboni mwa mama yake,alimshika kisigino kaka yake.Na alipokuwa mtu mzimaalishindana na Mungu.
5 Alipambana na malaika, akamshinda;alilia machozi na kuomba ahurumiwe.Huko Betheli, alikutana na Mungu,huko Mungu aliongea naye.
6 Mwenyezi-Mungu, wa majeshi,Mwenyezi-Mungu, ndilo jina lake.Lakini nyinyi mrudieni Mungu wenu.Zingatieni upendo na haki,mtumainieni Mungu wenu daima.
7 “Efraimu ni sawa na mfanyabiasharaatumiaye mizani danganyifu,apendaye kudhulumu watu.
8 Efraimu amesema,‘Mimi ni tajiri!Mimi nimejitajirisha!Hamna ubaya kupata faida.Hata hivyo, hilo si kosa!’”
9 Mwenyezi-Mungu asema, “Mimi ni Mwenyezi-Mungu, Mungu wako;mimi ndimi niliyekutoa nchini Misri!Mimi nitakukalisha tena katika mahema,kama ufanyavyo sasa kwa siku chache tu,wakati wa sikukuu ya vibanda.
10 Mimi niliongea na manabii;ni mimi niliyewapa maono mengi,na kwa njia yao natangaza mpango wangu.