7 Basi, nitakuwa kama simba kwenu nyote;nitawavizieni kama chui njiani.
8 Nitawarukieni kama dubualiyenyang'anywa watoto wake.Nitawararua vifua vyenuna kuwala papo hapo kama simba;nitawararua vipandevipande kama mnyama wa porini.
9 “Nitawaangamiza, enyi Waisraeli.Nani ataweza kuwasaidia?
10 Yuko wapi sasa mfalme wenu awaokoe?Wako wapi wale wakuu wenu wawalinde?Nyinyi ndio mlioomba:‘Tupatie mfalme na wakuu watutawale.’
11 Kwa hasira yangu mimi nikawapa mfalme,kisha nikamwondoa kwa ghadhabu yangu.
12 “Uovu wa Efraimu uko umeandikwa,dhambi yake imehifadhiwa ghalani.
13 Maumivu kama ya kujifungua mtoto yanamfikia.Lakini yeye ni mtoto mpumbavu;wakati ufikapo wa kuzaliwayeye hukataa kutoka tumboni kwa mama!