11 Nitazikomesha starehe zake zote,sikukuu zake za mwezi mwandamo na za Sabato,na sikukuu zote zilizoamriwa.
12 Nitaiharibu mizabibu yake na mitini,anayosema ni malipo kutoka kwa wapenzi wake.Nitaifanya iwe misitu,nao wanyama wa porini wataila.
13 Nitamlipiza sikukuu za Baali alizoadhimisha,muda alioutumia kuwafukizia ubani,akajipamba kwa pete zake na johari,na kuwaendea wapenzi wake,akanisahau mimi.Mimi Mwenyezi-Mungu nasema.
14 Kwa hiyo, nitamshawishi,nitampeleka jangwanina kusema naye kwa upole.
15 Huko nitamrudishia mashamba yake ya mizabibu,bonde la Akori nitalifanya lango la tumaini.Atanifuata kwa hiari kama alipokuwa kijana,kama wakati alipotoka katika nchi ya Misri.
16 “Mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Siku hiyo, wewe utaniita ‘Mume wangu,’ na sio tena ‘Baali wangu.’
17 Maana, nitalifanya jina la Baali lisitamkike tena kinywani mwako.