16 “Mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Siku hiyo, wewe utaniita ‘Mume wangu,’ na sio tena ‘Baali wangu.’
17 Maana, nitalifanya jina la Baali lisitamkike tena kinywani mwako.
18 Nitafanya agano na wanyama wa porini, ndege wa angani pamoja na vyote vitambaavyo, wasikuumize. Nitatokomeza upinde, upanga na silaha za vita katika nchi, na kukufanya uishi kwa usalama.
19 Nitakufanya mke wangu milele; uwe wangu kwa uaminifu na haki, kwa fadhili na huruma.
20 Naam, nitakuposa kwa uaminifu, nawe utanijua mimi Mwenyezi-Mungu.
21 “Siku hiyo, mimi Mwenyezi-Mungu nasema,nitaikubali haja ya mbingu ya kunyesha mvua,mbingu nazo zitaikubali haja ya ardhi.
22 Ardhi itaikubali haja ya nafaka, divai na mafuta,navyo vitatosheleza mahitaji ya Yezreeli.