20 Naam, nitakuposa kwa uaminifu, nawe utanijua mimi Mwenyezi-Mungu.
21 “Siku hiyo, mimi Mwenyezi-Mungu nasema,nitaikubali haja ya mbingu ya kunyesha mvua,mbingu nazo zitaikubali haja ya ardhi.
22 Ardhi itaikubali haja ya nafaka, divai na mafuta,navyo vitatosheleza mahitaji ya Yezreeli.
23 Nitamwotesha Yezreeli katika nchi;nitamhurumia ‘Asiyehurumiwa’,na wale walioitwa ‘Siwangu’,nitawaambia, ‘Nyinyi ni watu wangu.’Nao watasema, ‘Wewe ni Mungu wetu.’”