1 Msikilizeni Mwenyezi-Mungu,enyi Waisraeli.Mwenyezi-Mungu anawashutumu wakazi wa nchi hii.“Hamna tena uaminifu wala wema nchini;hamna anayemjua Mungu katika nchi hii.
2 Kuapa, uongo, mauaji, wizi na uzinzi huzuka humo.Umwagaji damu hufuatana mfululizo.
3 Kwa hiyo, nchi yote ni kame,wakazi wake wote wanaangamiapamoja na wanyama wa porini na ndege;hata samaki wa baharini wanaangamizwa.
4 “Lakini watu wasilaumiwe, wasishutumiwe;maana mimi nakushutumu wewe kuhani.
5 Wewe utajikwaa mchana,naye nabii atajikwaa pamoja nawe usiku.Nitamwangamiza mama yako Israeli.