2 Baada ya siku mbili, atatupa uhai tena,naam, siku ya tatu atatufufuaili tuweze kuishi pamoja naye.
3 Basi tumtambue,tujitahidi kumjua Mwenyezi-Mungu.Kuja kwake ni hakika kama alfajiri,yeye atatujia kama manyunyu,kama mvua za masika ziinyweshayo ardhi.’”
4 Lakini Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Nitakutendea nini ee Efraimu?Nikufanyie nini ee Yuda?Upendo wenu kwangu ni kama ukungu wa asubuhi,kama umande unaotoweka upesi.
5 Ndiyo maana nimewavamia kwa njia ya manabii,nimewaangamiza kwa maneno yangu,hukumu yangu huchomoza kama pambazuko.
6 Maana ninachotaka kwenu ni upendo na si tambiko,Kumjua Mungu na si kutoa sadaka za kuteketezwa.
7 “Lakini mlilivunja agano langukama mlivyofanya mjini Adamu;huko walinikosea uaminifu.
8 Gileadi ni mji wa waovu,umetapakaa damu.