18 Wewe, ee Mwenyezi-Mungu,watawala milele na milele.”
19 Wakati farasi wa Farao na magari yake pamoja na wapandafarasi wake walipoingia mahali pakavu baharini, Mwenyezi-Mungu aliyarudisha maji ya bahari yakawafunika. Lakini Waisraeli waliendelea kutembea pakavu katikati ya bahari.
20 Basi nabii Miriamu, dada yake Aroni, akachukua kingoma mkononi, na wanawake wengine wote wakamfuata wakiwa na vingoma vyao wakicheza.
21 Miriamu akawaongoza kwa kuimba,“Mwimbieni Mwenyezi-Mungu kwani ameshinda kwa fahari,farasi na mpandafarasi wake amewatosa baharini.”
22 Kisha, Mose aliwaongoza Waisraeli kutoka bahari ya Shamu, wakaenda mpaka jangwa la Shuri. Walisafiri kwa muda wa siku tatu jangwani bila kuona maji yoyote.
23 Walipofika mahali panapoitwa Mara, hawakuweza kuyanywa maji ya Mara kwa sababu yalikuwa machungu. Kwa sababu hiyo mahali hapo pakaitwa Mara.
24 Basi, watu wote wakamlalamikia Mose wakisema, “Sasa tutakunywa nini?”