13 Baada ya kumzaa Shela, Arfaksadi aliishi miaka 403 na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike.
14 Shela alipokuwa na umri wa miaka 30, alimzaa Eberi.
15 Baada ya kumzaa Eberi, Shela aliishi miaka 403 na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike.
16 Eberi alipokuwa na umri wa miaka 34, alimzaa Pelegi.
17 Baada ya kumzaa Pelegi, Eberi aliishi miaka 430 na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike.
18 Pelegi alipokuwa na umri wa miaka 30, alimzaa Reu.
19 Baada ya kumzaa Reu, Pelegi aliishi miaka 209 na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike.