18 Siku hiyo, Mwenyezi-Mungu akafanya agano na Abramu akisema, “Wazawa wako ninawapa nchi hii, toka mto wa Misri hadi ule mto mkubwa wa Eufrate,
19 yaani nchi za Wakeni, Wakenizi, Wakadmoni,
20 Wahiti, Waperizi, Warefai,
21 Waamori, Wakanaani, Wagirgashi na Wayebusi.”