2 Nami nitafanya agano nawe na kuwazidisha wazawa wako.”
3 Hapo Abramu akasujudu. Naye Mungu akamwambia,
4 “Ninafanya agano hili nawe: Utakuwa baba wa mataifa mengi.
5 Tangu sasa, hutaitwa tena Abramu, bali utaitwa Abrahamu, maana nimekufanya kuwa baba wa mataifa mengi.
6 Nitakufanya uwe na wazawa wengi sana; kwako nitazusha mataifa mengi na wafalme.
7 Nitalithibitisha agano langu nawe, wazawa wako na vizazi vyao vyote milele; tena nitakuwa Mungu wako na Mungu wa wazawa wako milele.
8 Nitakupa wewe na wazawa wako nchi hii ambamo unaishi kama mgeni; yaani nchi yote ya Kanaani iwe mali yenu milele; nami nitakuwa Mungu wao.”