1 Hivyo ndivyo mbingu na dunia zilivyokamilika pamoja na vitu vyote vilivyomo.
2 Siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyofanya; siku hiyo ya saba Mungu akapumzika baada ya kazi yake yote aliyofanya.
3 Mungu akaibariki siku ya saba na kuitakasa, kwa kuwa siku hiyo Mungu alipumzika baada ya kazi yake yote ya kuumba.
4 Hivyo ndivyo mbingu na dunia zilivyoumbwa.Siku ile Mwenyezi-Mungu alipoziumba mbingu na dunia,