20 Basi, akafanya haraka, akawamiminia ngamia maji ya mtungi wake katika hori, akakimbia kisimani kuteka maji mengine na kuwanywesha ngamia wake wote.
21 Yule mtu akawa anamtazama kwa makini bila kusema lolote, apate kufahamu kama Mwenyezi-Mungu ameifanikisha safari yake au sivyo.
22 Ngamia walipotosheka kunywa maji, yule mtu akampa huyo msichana pete ya dhahabu yenye uzito upatao gramu sita, na bangili mbili za dhahabu za gramu kumi kila moja.
23 Akamwuliza, “Niambie tafadhali: Wewe ni binti nani? Je, kuna nafasi ya kulala nyumbani kwenu?”
24 Rebeka akajibu, “Mimi ni binti Bethueli, mwana wa Milka, mkewe Nahori.
25 Kwetu kuna majani na malisho ya kutosha na mahali pa kulala wageni.”
26 Ndipo yule mtu akainamisha kichwa chake, akamwabudu Mwenyezi-Mungu