30 Dishoni, Eseri na Dishani; kila mmoja wao akiwa mkuu wa kabila lake katika nchi ya Seiri.
31 Wafuatao ni wafalme waliotawala nchi ya Edomu, kabla mfalme yeyote hajawatawala Waisraeli:
32 Bela mwana wa Beori alitawala nchi ya Edomu akiwa na makao yake makuu katika mji wa Dinhaba.
33 Bela alipofariki, Yobabu mwana wa Zera kutoka Bosra alitawala badala yake.
34 Yobabu alipofariki, Hushamu wa nchi ya Watemani, alitawala badala yake.
35 Hushamu alipofariki, Hadadi mwana wa Bedadi alitawala badala yake, makao yake makuu yakiwa katika mji wa Avithi. Huyu ndiye aliyewapiga na kuwashinda Wamidiani katika nchi ya Moabu.
36 Hadadi alipofariki, Samla kutoka Masreka, alitawala badala yake.