29 Alimwita mtoto huyo Noa, akisema, “Mtoto huyu ndiye atakayetufariji kutokana na kazi yetu ngumu tunayofanya kwa mikono yetu katika ardhi aliyoilaani Mwenyezi-Mungu.”
30 Baada ya kumzaa Noa, Lameki aliishi miaka 595 na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike.
31 Lameki alifariki akiwa na umri wa miaka 777.
32 Noa alipokuwa na umri wa miaka 500, alimzaa Shemu na Hamu na Yafethi.