42 Basi Mungu akaghairi, akawaacha ili waliabudu jeshi la mbinguni, kama ilivyoandikwa katika chuo cha manabii,Je! Mlinitolea mimi dhabihu na sadakaMiaka arobaini katika jangwa, enyi nyumba ya Israeli?
43 Nanyi mlichukua hema ya Moleki,Na nyota za mungu wenu Refani,Sanamu mlizozifanya ili kuziabudu;Nami nitawafahamisha mwende mbali kupita Babeli.
44 Ile hema ya ushahidi ilikuwa pamoja na baba zetu jangwani, kama alivyoagiza yeye aliyesema na Musa, ya kwamba aifanye sawasawa na mfano ule aliouona;
45 ambayo baba zetu, kwa kupokezana, wakaiingiza pamoja na Yoshua katika milki ya Mataifa wale, ambao Mungu aliwafukuza mbele ya baba zetu, mpaka siku za Daudi;
46 aliyepata fadhili mbele za Mungu, naye aliomba ampatie Mungu wa Yakobo maskani.
47 Lakini Sulemani alimjengea nyumba.
48 Ila Yeye aliye juu hakai katika nyumba zilizofanywa kwa mikono, kama vile asemavyo nabii,