1 Nafsi yangu inachoka na maisha yangu;Sitajizuia na kuugua kwangu;Nitanena kwa uchungu wa roho yangu.
2 Nitamwambia Mungu, Usinihukumie makosa;Nionyeshe sababu ya wewe kushindana nami.
3 Je! Ni vema kwako wewe kuonea,Na kuidharau kazi ya mikono yako,Na kuyaangazia mashauri ya waovu?
4 Je! Wewe una macho ya kimwili,Au je! Waona kama aonavyo binadamu?
5 Je! Siku zako ni kama siku za mtu,Au je! Miaka yako ni kama siku za mtu,
6 Hata ukauliza-uliza habari za uovu wangu,Na kuitafuta dhambi yangu,