4 Je! Wewe una macho ya kimwili,Au je! Waona kama aonavyo binadamu?
5 Je! Siku zako ni kama siku za mtu,Au je! Miaka yako ni kama siku za mtu,
6 Hata ukauliza-uliza habari za uovu wangu,Na kuitafuta dhambi yangu,
7 Ujapojua ya kuwa mimi si mwovu;Wala hapana awezaye kuokoa na mkono wako?
8 Mikono yako imeniumba na kunifinyanga;Nawe utageuka na kuniangamiza?
9 Kumbuka, nakusihi ulivyonifinyanga kama vile udongo;Nawe, je! Utanirudisha uvumbini tena?
10 Je! Wewe hukunimimina kama maziwa,Na kunigandisha mfano wa jibini?