16 Hiyo pepo ilisimama kimya, nisiweze kutambua sura zake,Mfano ulikuwa mbele ya macho yangu;Kulikuwa kimya, nami nilisikia sauti, ikinena,
17 Je! Binadamu atakuwa na haki kuliko Mungu?Je! Mtu atakuwa safi kuliko Muumba wake?
18 Tazama, yeye hawategemei watumishi wake;Na malaika zake huwahesabia upuzi;
19 Je! Si zaidi sana hao wakaao katika nyumba za udongo,Ambazo misingi yao i katika mchanga,Hao waliosetwa mbele ya nondo!
20 Kati ya asubuhi na jioni huvunjwa-vunjwa;Waangamia milele wala hapana atiaye moyoni.
21 Je! Kamba ya hema yao haikung’olewa ndani yao?Wafa, kisha hali hawana akili.