1 Je! Mtu hana wakati wake wa vita juu ya nchi?Na siku zake, je! Si kama siku za mwajiriwa?
2 Kama mtumishi atamaniye sana kile kivuli,Kama mwajiriwa anayetazamia mshahara wake;
3 Ni vivyo nami nimepewa miezi ya ubatili iwe fungu langu,Nami nimeandikiwa masiku yenye kuchokesha.
4 Hapo nilalapo chini, nasema,Nitaondoka lini? Lakini usiku huwa mrefu;Nami nimejawa na kujitupa huku na huku hata kupambazuke.
5 Mwili wangu unavikwa mabuu na madongoa ya udongo;Ngozi yangu hufumba, kisha ikatumbuka tena.