5 Mwili wangu unavikwa mabuu na madongoa ya udongo;Ngozi yangu hufumba, kisha ikatumbuka tena.
6 Siku zangu hupita upesi kuliko chombo cha kufumia,Nazo zapita pasipokuwa na matumaini.
7 Kumbuka ya kwamba maisha yangu ni upepo;Jicho langu halitaona mema tena.
8 Jicho lake huyo anionaye halitaniangalia tena;Macho yako yatanielekea, lakini sitakuwapo.
9 Kama vile wingu likomavyo na kutoweka,Ni vivyo huyo ashukaye kuzimuni hatazuka tena kabisa.
10 Hatarudi tena nyumbani kwake,Wala mahali pake hapatamjua tena.
11 Kwa hiyo sitakizuia kinywa changu;Nitanena kwa mateso ya roho yangu;Nitalia kwa uchungu wa nafsi yangu.