3 Mimi mwenyewe nimewaamuru watu wangu waliowekwa wakfu kwangu, naam, nimewaita watu wangu walio hodari kwa ajili ya hasira yangu, watu wangu wenye kutakabari.
4 Kelele milimani kama kelele za watu wengi sana; kelele za falme za mataifa waliokutana pamoja; BWANA wa majeshi anapanga jeshi kwa vita;
5 watu waliotoka katika nchi iliyo mbali, tokea upande wa mwisho wa mbingu; naam, BWANA na silaha za ghadhabu yake, ili aiangamize nchi yote.
6 Pigeni kelele za hofu; maana siku ya BWANA i karibu; itanyesha kama maangamizi yatokayo kwa Mwenyezi Mungu.
7 Kwa sababu hiyo mikono yote italegea, na moyo wa kila mtu utayeyuka.
8 Nao watafadhaika; watashikwa na utungu na maumivu; watakuwa na utungu kama mwanamke aliye karibu na kuzaa; watakodoleana macho; nyuso zao zitakuwa ni nyuso za moto.
9 Tazama, siku ya BWANA inakuja, siku kali, ya hasira na ghadhabu kuu, ili iifanye nchi kuwa ukiwa, na kuwaharibu watu wake, wenye dhambi, wasikae ndani yake.