14 Nitapaa kupita vimo vya mawingu,Nitafanana na yeye Aliye juu.
15 Lakini utashushwa mpaka kuzimu;Mpaka pande za mwisho za shimo.
16 Wao wakuonao watakukazia macho,Watakuangalia sana, wakisema,Je! Huyu ndiye aliyeitetemesha dunia,Huyu ndiye aliyetikisa falme;
17 Aliyeufanya ulimwengu ukiwa, akaipindua miji yake;Asiyewafungua wafungwa wake waende kwao?
18 Wafalme wote wa mataifa wamezikwa wote kwa heshima,Kila mmoja ndani ya nyumba yake mwenyewe;
19 Bali wewe umetupwa mbali na kaburi lako,Kama chipukizi lililochukiza kabisa;Kama vazi la wale waliouawa,Wale waliochomwa kwa upanga,Wale washukao mpaka misingi ya shimo;Kama mzoga uliokanyagwa chini ya miguu.
20 Hutaungamanishwa pamoja nao katika mazishi,Kwa maana umeiharibu nchi yako,Umewaua watu wako;Kizazi chao watendao uovu hakitatajwa milele.