17 Aliyeufanya ulimwengu ukiwa, akaipindua miji yake;Asiyewafungua wafungwa wake waende kwao?
18 Wafalme wote wa mataifa wamezikwa wote kwa heshima,Kila mmoja ndani ya nyumba yake mwenyewe;
19 Bali wewe umetupwa mbali na kaburi lako,Kama chipukizi lililochukiza kabisa;Kama vazi la wale waliouawa,Wale waliochomwa kwa upanga,Wale washukao mpaka misingi ya shimo;Kama mzoga uliokanyagwa chini ya miguu.
20 Hutaungamanishwa pamoja nao katika mazishi,Kwa maana umeiharibu nchi yako,Umewaua watu wako;Kizazi chao watendao uovu hakitatajwa milele.
21 Fanyeni tayari machinjo kwa watoto wake.Kwa sababu ya uovu wa baba zao;Wasije wakainuka na kuitamalaki nchi,Na kuujaza miji uso wa ulimwengu.
22 Nami nitainuka, nishindane nao; asema BWANA wa majeshi; na katika Babeli nitang’oa jina na mabaki, mwana na mjukuu; asema BWANA.
23 Tena nitaifanya hiyo nchi kuwa makao ya nungu, na maziwa ya maji; nami nitaifagilia mbali kwa ufagio wa uharibifu; asema BWANA wa majeshi.