5 Kwa kuwa amewashusha wakaao juu,Mji ule ulioinuka, aushusha,Aushusha hata nchi, auleta hata mavumbini.
6 Mguu utaukanyaga chini,Naam, miguu yao walio maskini,Na hatua zao walio wahitaji.
7 Njia yake mwenye haki ni unyofu;Wewe uliye mnyofu wainyosha njia ya mwenye haki.
8 Naam, katika njia ya hukumu zakoSisi tumekungoja, Ee BWANA;Shauku ya nafsi zetu inaelekeaJina lako na ukumbusho wako.
9 Kwa nafsi yangu nimekutamani wakati wa usiku;Naam, kwa nafsi yangu ndani yangu nitakutafuta mapema;Maana hukumu zako zikiwapo duniani,Watu wakaao duniani hujifunza haki.
10 Mtu mbaya ajapofadhiliwa,Hata hivyo hatajifunza haki;Katika nchi ya unyofu atatenda udhalimu,Wala hatauona utukufu wa BWANA.
11 BWANA, mkono wako umeinuliwa, lakini hawaoni; lakini watauona wivu wako kwa ajili ya watu wako, nao watatahayari; naam, moto utawala adui zako.