1 Katika siku hiyo BWANA, kwa upanga wake ulio mkali, ulio mkubwa, ulio na nguvu, atamwadhibu lewiathani, nyoka yule mwepesi, na lewiathani, nyoka yule mwenye kuzonga-zonga; naye atamwua yule joka aliye baharini.
2 Katika siku hiyo; Shamba la mizabibu la mvinyo, liimbieni.
3 Mimi, BWANA, nalilinda,Nitalitia maji kila dakika,Asije mtu akaliharibu;Usiku na mchana nitalilinda.
4 Hasira sinayo ndani yangu;Kama mibigili na miiba ingekuwa mbele zangu,Ningepanga vita juu yake,Ningeiteketeza yote pamoja.