15 Mimi ni BWANA, Mtakatifu wenu, Muumba wa Israeli, mfalme wenu.
16 BWANA asema hivi, yeye afanyaye njia katika bahari; na mahali pa kupita katika maji yenye nguvu;
17 atoaye gari na farasi, jeshi la askari na uwezo; wamelala, hawataondoka; wametoweka, wamezimwa mfano wa utambi.
18 Msiyakumbuke mambo ya kwanza, wala msiyatafakari mambo ya zamani.
19 Tazama, nitatenda neno jipya; sasa litachipuka; je! Hamtalijua sasa? Nitafanya njia hata jangwani, na mito ya maji nyikani.
20 Wanyama wa kondeni wataniheshimu, mbweha pia na mbuni; kwa sababu nimewapa maji jangwani, na mito nyikani, ili kuwanywesha watu wangu, wateule wangu;
21 watu wale niliojiumbia nafsi yangu, ili wazitangaze sifa zangu.