14 Yeye aliyehamishwa na kufungwa atafunguliwa kwa haraka; wala hatakufa na kushuka shimoni, wala chakula chake hakitapunguka.
15 Maana mimi ni BWANA, Mungu wako, niichafuaye bahari, mawimbi yake yakavuma.
16 BWANA wa majeshi ndilo jina lake. Nami nimetia maneno yangu kinywani mwako, nami nimekusitiri katika kivuli cha mkono wangu, ili nizipande mbingu, na kuiweka misingi ya dunia, na kuuambia Sayuni, Ninyi ni watu wangu.
17 Amka, amka, simama, Ee Yerusalemu,Wewe uliyenywea, mkononi mwa BWANA,Kikombe cha hasira yake;Bakuli la kikombe cha kulevya-levyaUmelinywea na kulimaliza.
18 Hapana hata mmoja wa kumwongozaMiongoni mwa wana wote aliowazaa,Wala hapana hata mmoja wa kumshika mkonoMiongoni mwa wana wote aliowalea.
19 Mambo haya mawili yamekupata;Ni nani awezaye kukusikitikia?Ukiwa na uharibifu, na njaa na upanga;Niwezeje kukutuliza?
20 Wana wako wamezimia,Wamelala penye pembe za njia kuu zoteKama kulungu wavuni;Wamejaa hasira ya BWANA,Lawama ya Mungu wako.