1 Amka, amka, jivike nguvu zako, Ee Sayuni;Jivike mavazi yako mazuri,Ee Yerusalemu, mji mtakatifu;Kwa maana tokea sasa hataingia ndani yakoAsiyetahiriwa, wala aliye najisi.
2 Jikung’ute mavumbi; uondoke,Uketi, Ee Yerusalemu;Jifungulie vifungo vya shingo yako,Ee binti Sayuni uliyefungwa.
3 Maana BWANA asema hivi, Mliuzwa bure; nanyi mtakombolewa bila fedha.
4 Maana Bwana MUNGU asema hivi, Watu wangu hapo kwanza walishuka Misri ili wakae huko hali ya ugeni; na Mwashuri akawaonea bila sababu.
5 Basi sasa, nafanya nini hapa, asema BWANA, ikiwa watu wangu wamechukuliwa bure? Hao wanaowatawala wanapiga yowe, asema BWANA, na jina langu linatukanwa daima mchana kutwa.
6 Kwa hiyo watu wangu watalijua jina langu kwa hiyo watajua siku ile ya kuwa mimi ndimi ninenaye; tazama ni mimi.