1 Ondoka, uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja,Na utukufu wa BWANA umekuzukia.
2 Maana, tazama, giza litaifunika dunia,Na giza kuu litazifunika kabila za watu;Bali BWANA atakuzukia wewe,Na utukufu wake utaonekana juu yako.
3 Na mataifa wataijilia nuru yako,Na wafalme kuujia mwanga wa kuzuka kwako.
4 Inua macho yako, utazame pande zote;Wote wanakusanyana; wanakujia wewe;Wana wako watakuja kutoka mbali.Na binti zako watabebwa nyongani.
5 Ndipo utakapoona na kutiwa nuru,Na moyo wako utatetemeka na kukunjuka;Kwa kuwa wingi wa bahari utageuzwa kukujia,Utajiri wa mataifa utakuwasilia.