3 Umeliongeza taifa, umezidisha furaha yao;Wanafurahi mbele zako,Kama furaha ya wakati wa mavuno,Kama watu wafurahivyo wagawanyapo nyara.
4 Kwa maana umeivunja nira ya mzigo wake, na gongo la bega lake, na fimbo yake yeye aliyemwonea, kama katika siku ya Midiani.
5 Maana silaha zote za mtu mwenye silaha wakati wa mshindo, na mavazi yaliyofingirishwa katika damu, yatakuwa tayari kuteketezwa, yatakuwa kuni za kutiwa motoni.
6 Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa,Tumepewa mtoto mwanamume;Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake;Naye ataitwa jina lake,Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu,Baba wa milele, Mfalme wa amani.
7 Maongeo ya enzi yake na amaniHayatakuwa na mwisho kamwe,Katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake;Kuuthibitisha na kuutegemezaKwa hukumu na kwa haki,Tangu sasa na hata milele.Wivu wa BWANA wa majeshi ndio utakaotenda hayo.
8 Bwana alimpelekea Yakobo neno, likamfikilia Israeli.
9 Nao watu wote watajua, yaani, Efraimu na yeye akaaye Samaria, wasemao kwa kiburi na kwa kujisifu nafsi zao,