3 Tengenezeni kigao na ngao, mkakaribie ili kupigana.
4 Watandikeni farasi; pandeni, enyi mpandao farasi; simameni na chapeo zenu, isugueni mikuki; zivaeni dirii.
5 Nimeyaona haya kwa sababu gani? Wamefadhaika, wamerudi nyuma; mashujaa wao wamevunjika-vunjika; wanakimbia upesi sana, hawatazami nyuma; hofu ziko pande zote; asema BWANA.
6 Mtu mwepesi asikimbie, wala shujaa asiokoke; pande za kaskazini karibu na mto Frati wamejikwaa na kuanguka.
7 Nani huyu ajiinuaye kama mto Nile,Ambaye maji yake yanajirusha kama mito?
8 Misri anajiinua kama mto Nile,Na maji yake yanajirusha kama mito;Asema, Nitajiinua, nitaifunikiza nchi;Nitauharibu mji na hao wakaao ndani yake.
9 Haya! Pandeni, enyi farasi;Jihimizeni, enyi magari ya vita;Mashujaa nao na watoke njeKushi na Puti, watumiao ngao;Nao Waludi, washikao uta na kuupeta.