8 Nitawang'oa wakazi wa mji wa Ashdodi,pamoja na mtawala wa Ashkeloni.Nitanyosha mkono dhidi ya Ekroni,nao Wafilisti wote waliosalia wataangamia.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
9 Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Watu wa Tiro wametenda dhambi tena na tena,kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu.Walichukua mateka kabila zima hadi Edomu,wakaukiuka mkataba wa urafiki waliokuwa wamefanya.
10 Basi, nitazishushia moto kuta za mji wa Tiro,na kuziteketeza kabisa ngome zake.”
11 Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Watu wa Edomu wametenda dhambi tena na tena,kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu.Waliwawinda ndugu zao Waisraeli kwa mapanga,wakaitupilia mbali huruma yao yote ya kindugu.Hasira yao haikuwa na kikomo,waliiacha iwake daima.
12 Basi, nitaushushia moto mji wa Temani,na kuziteketeza kabisa ngome za Bosra.”
13 Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Watu wa Amoni wametenda dhambi tena na tena,kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu.Katika vita vyao vya kupora nchi zaidi,waliwatumbua wanawake waja wazito nchini Gileadi.
14 Basi, nitazishushia moto kuta za mji wa Raba,na kuziteketeza kabisa ngome zake.Siku hiyo ya vita patakuwa na makelele mengi,nayo mapambano yatakuwa makali kama tufani.