5 Toeni tambiko ya shukrani ya mikate iliyochachushwa.Tangazeni popote kwamba mmetoa kwa hiari;kwani ndivyo mnavyopenda kufanya!Mimi Bwana Mungu nimenena.
6 “Mimi niliwanyima chochote cha kutafuna,nikasababisha ukosefu wa chakula popote.Hata hivyo hamkunirudia.Nasema mimi Mwenyezi-Mungu.
7 “Tena niliwanyima mvuamiezi mitatu tu kabla ya mavuno.Niliunyeshea mvua mji mmoja,na mji mwingine nikaunyima.Shamba moja lilipata mvua,na lingine halikupata, likakauka.
8 Watu wa miji miwili, mitatu wakakimbilia mji mwingine,wapate maji, lakini hayakuwatosha.Hata hivyo hamkunirudia.Nasema mimi Mwenyezi-Mungu.
9 “Niliwapiga pigo la ukame na ukungu;nikakausha bustani na mashamba yenu ya mizabibu;nzige wakala mitini na mizeituni yenu.Hata hivyo hamkunirudia.Nasema mimi Mwenyezi-Mungu.
10 “Niliwaleteeni ugonjwa wa taunikama ule nilioupelekea Misri.Niliwaua vijana wenu vitani,nikawachukua farasi wenu wa vita.Maiti zilijaa katika kambi zenu,uvundo wake ukajaa katika pua zenu.Hata hivyo hamkunirudia.Nasema mimi Mwenyezi-Mungu.
11 “Niliwaangusha baadhi yenu kwa maangamizikama nilivyoangamiza Sodoma na Gomora.Wale walionusurika miongoni mwenu,walikuwa kama kijiti kilichookolewa motoni.Hata hivyo hamkunirudia.Nasema mimi Mwenyezi-Mungu.