20 ili mpate kufuata kanuni zangu na kuyatii maagizo yangu; nanyi mtakuwa watu wangu nami nitakuwa Mungu wenu.
21 Lakini hao ambao moyo wao umeambatana na vitu najisi na machukizo yao, nitawaadhibu kadiri ya mienendo yao. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
22 Hapo wale viumbe waliyakunjua mabawa yao na kuanza kuruka pamoja na yale magurudumu yaliyokuwa kando yao, nao utukufu wa Mungu wa Israeli ulikuwa juu yao.
23 Basi, utukufu wa Mwenyezi-Mungu ukapaa juu kutoka katikati ya mji, ukasimama juu ya mlima ulio upande wa mashariki wa mji.
24 Nikiwa katika maono hayo, roho ya Mungu ilininyanyua na kunipeleka mpaka nchi ya Wakaldayo, kwa watu walioko uhamishoni huko. Kisha maono hayo yakatoweka.
25 Hapo nikawaeleza wale waliokuwa uhamishoni mambo yote aliyonionesha Mwenyezi-Mungu.