1 Neno la Mwenyezi-Mungu lilinijia:
2 “Wewe mtu! Je, mti wa mzabibu ni bora kuliko miti mingine msituni?
3 Je, mti wake wafaa kutengenezea kitu chochote? Je, watu huweza kutengeneza kigingi kutoka mti huo ili waweze kutundikia vitu?
4 Huo wafaa tu kuwashia moto. Tena moto unapoteketeza sehemu yake ya mwanzo na ya mwisho na kuikausha sehemu ya katikati, je, hiyo yafaa kwa kitu chochote?
5 Ulipokuwa haujachomwa ulikuwa haufai kitu, sembuse sasa baada ya kuteketezwa kwa moto na kuwa makaa! Haufai kitu kabisa.
6 Basi, mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Kama vile nilivyoutoa mti wa mzabibu kati ya miti ya msituni, ukateketezwa motoni, ndivyo nilivyotoa wakazi wa Yerusalemu.