1 Mungu aliniambia niimbe utenzi huu wa maombolezo kuhusu wakuu wa Israeli:
2 Mama yenu alikuwa simba wa faharimiongoni mwa simba wengine.Alikaa kati ya simba vijana,akawalisha watoto wake.
3 Alimlea mtoto mmojawapo wa watoto wake,mtoto huyo naye akawa simba kijana hodari.Akajifunza kwa mama yake kuwinda,akawa simba mla watu.
4 Mataifa yakapiga mbiu ya hatari dhidi yake,wakamnasa katika mtego wao,wakampeleka kwa ndoana mpaka Misri.
5 Mama yake alipoona kuwa amechoka kungoja,matumaini ya kumpata yamekwisha,alimchukua mtoto wake mwingine,akamfanya simba kijana hodari.
6 Huyo alipokuwa amekua,akaanza kuzurura na simba wengine.Naye pia akajifunza kuwinda,akawa simba mla watu.