11 Ulikuwa na matawi yenye nguvu,ambayo yalikuwa fimbo za kifalme.Mzabibu huo ulikua kupita miti mingine,watu waliusifu ukubwa wa shina lakena wingi wa matawi yake.
12 Lakini ulingolewa kwa hasiraukatupwa chini ardhini;upepo wa mashariki ukaukausha,matunda yake yakapukutika;matawi yake yenye nguvu yalikaushwa,nao moto ukauteketeza.
13 Na sasa umepandikizwa jangwani,katika nchi kame isiyo na maji.
14 Lakini moto umetoka kwenye shina lake,umeyateketeza matawi na matunda yake.Matawi yake kamwe hayatakuwa na nguvu,wala hayatakuwa fimbo za kifalme.Huo umekuwa wimbo wa maombolezo; ndivyo unavyoimbwa daima.