3 Alimlea mtoto mmojawapo wa watoto wake,mtoto huyo naye akawa simba kijana hodari.Akajifunza kwa mama yake kuwinda,akawa simba mla watu.
4 Mataifa yakapiga mbiu ya hatari dhidi yake,wakamnasa katika mtego wao,wakampeleka kwa ndoana mpaka Misri.
5 Mama yake alipoona kuwa amechoka kungoja,matumaini ya kumpata yamekwisha,alimchukua mtoto wake mwingine,akamfanya simba kijana hodari.
6 Huyo alipokuwa amekua,akaanza kuzurura na simba wengine.Naye pia akajifunza kuwinda,akawa simba mla watu.
7 Aliziandama ngome za watuna kuiharibu miji yao.Nchi ikatishika pamoja na wakazi wake,kwa sauti ya kunguruma kwake.
8 Mataifa yakamkabili kutoka mkoani mwao kote,wakatandaza wavu wao juu yake,naye akanaswa katika mtego wao.
9 Kwa ndoana wakamtia katika kizimba chao,wakampeleka kwa mfalme wa Babuloni.Huko, wakamtia gerezani,ili ngurumo yake isisikike tenajuu ya milima ya Israeli.