28 Mlio wa mabaharia wako utakaposikika,nchi za pwani zitatetemeka.
29 Hapo wapiga makasia wotewataziacha meli zao.Wanamaji na manahodha watakaa pwani.
30 Wataomboleza kwa uchungu wa moyo juu yako,na kulia kwa uchungu mkubwa;watajitupia mavumbi vichwani mwaona kugaagaa kwenye majivu.
31 Wamejinyoa vichwa kwa ajili yakona kuvaa mavazi ya gunia.Watalia kwa uchungu wa moyo juu yako.
32 Wataimba wimbo wa ombolezo juu yako;‘Nani aliyepata kuangamizwa kama Tirokatikati ya bahari?’
33 Bidhaa zako zilipowasili nchi za ngambo,ulitosheleza mahitaji ya watu wengi!Kwa wingi wa utajiri wa bidhaa zakouliwatajirisha wafalme wa dunia.
34 Lakini sasa umevunjikia baharini;umeangamia katika vilindi vya maji.Shehena yako na jamii ya mabahariavimezama pamoja nawe.