31 Wamejinyoa vichwa kwa ajili yakona kuvaa mavazi ya gunia.Watalia kwa uchungu wa moyo juu yako.
32 Wataimba wimbo wa ombolezo juu yako;‘Nani aliyepata kuangamizwa kama Tirokatikati ya bahari?’
33 Bidhaa zako zilipowasili nchi za ngambo,ulitosheleza mahitaji ya watu wengi!Kwa wingi wa utajiri wa bidhaa zakouliwatajirisha wafalme wa dunia.
34 Lakini sasa umevunjikia baharini;umeangamia katika vilindi vya maji.Shehena yako na jamii ya mabahariavimezama pamoja nawe.
35 Wakazi wote wa visiwaniwamepigwa na bumbuazi juu yako;wafalme wao wameogopa kupindukia,nyuso zimekunjamana kwa huzuni.
36 Wachuuzi wa mataifa watakufyonya!Umeufikia mwisho wa kutisha,na hutakuwapo tena milele!”