1 Mnamo siku ya kwanza ya mwezi wa tatu, mwaka wa kumi na moja tangu uhamisho wetu, neno la Mwenyezi-Mungu lilinijia:
2 “Wewe mtu! Mwambie hivi Farao mfalme wa Misri na watu wake wote:Wewe wafanana na nini kwa ukuu wako?
3 Wewe ni kama mwerezi wa Lebanoniwenye matawi mazuri na majani mengi na shina refu.Kilele chake kinafika hata mawinguni.
4 Maji yaliustawisha,vilindi vya maji viliulisha.Mito ilibubujika mahali ulipoota,ikapeleka vijito kwenye miti yote ya msituni.