21 kikosi chake kulingana na hesabu kitakuwa watu 32,000.
22 Hatimaye kabila la Benyamini: Kiongozi wake ni Abidani, mwana wa Gideoni,
23 kikosi chake kulingana na hesabu kitakuwa na watu 35,400.
24 Jumla ya watu watakaokuwa katika kambi ya Efraimu kulingana na makundi yao ni watu 108,100. Kundi hili la Efraimu litakuwa katika msafara wa tatu.
25 “Kwa upande wa kaskazini, watapiga kambi katika makundi yao wale walio chini ya bendera ya Dani, kiongozi wao atakuwa Ahiezeri, mwana wa Amishadai,
26 kikosi chake kulingana na hesabu kitakuwa na watu 62,700.
27 Kisha wale watakaopiga kambi baada yao watakuwa watu wa kabila la Asheri, kiongozi wao akiwa Pagieli mwana wa Okrani,