27 Kisha wale watakaopiga kambi baada yao watakuwa watu wa kabila la Asheri, kiongozi wao akiwa Pagieli mwana wa Okrani,
28 kikosi chake kulingana na hesabu kitakuwa na watu 41,500.
29 “Hatimaye watu wa kabila la Naftali, kiongozi wake akiwa Ahira mwana wa Enani,
30 kikosi chake kulingana na hesabu, kitakuwa na watu 53,400.
31 Jumla ya watu watakaokuwa katika kambi ya Dani kulingana na makundi yao ni watu 157,600. Kundi hili la Dani litakuwa katika msafara wa mwisho, bendera baada ya bendera.”
32 Hao ndio Waisraeli waliohesabiwa kulingana na koo zao, katika kambi na vikosi vyao; wote walikuwa 603,550.
33 Lakini Walawi hawakuhesabiwa miongoni mwa watu wa Israeli kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.