26 “Mnamo siku ya kwanza ya sikukuu ya majuma wakati mnapomtolea Mwenyezi-Mungu malimbuko ya nafaka zenu, mtafanya mkutano mtakatifu; msifanye kazi.
27 Mtatoa sadaka ya kuteketezwa, harufu nzuri ya kumpendeza Mwenyezi-Mungu: Fahali wachanga wawili, kondoo dume mmoja, na wanakondoo saba madume wa mwaka mmoja, wote hao wawe hawana dosari.
28 Sadaka ya nafaka itakayoandamana nazo itakuwa ya unga safi uliochanganywa na mafuta kilo tatu kwa kila fahali, kilo mbili kwa kila kondoo dume,
29 na kilo moja kwa kila mwanakondoo.
30 Mtatoa pia beberu mmoja kuwa sadaka ya kuondoa dhambi ili kuwafanyia upatanisho.
31 Mtatoa vitu hivi licha ya ile sadaka ya kuteketezwa ya kawaida pamoja na sadaka yake ya kinywaji.