30 Kutoka lile fungu la jumuiya nzima, chukua sehemu moja ya kila hamsini, iwe ni watu, ng'ombe, punda, kondoo na mbuzi. Hivyo utawapa Walawi ambao wana wajibu wa kuhudumu katika hema la Mwenyezi-Mungu.”
31 Mose na kuhani Eleazari walifanya kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.
32 Nyara walizoteka wanajeshi zilikuwa: Kondoo 675,000,
33 ng'ombe 72,000,
34 punda 61,000,
35 na wasichana ambao hawakuwa wamelala na mwanamume 32,000.
36 Nusu yake, sehemu ambayo iligawiwa wanajeshi waliokwenda vitani, ilikuwa kondoo 337,500,