9 Waisraeli waliteka nyara: Ng'ombe, kondoo na mali yao yote.
10 Miji yao yote, makazi yao na kambi zao zote waliziteketeza kwa moto.
11 Walichukua nyara zote na mateka yote, ya watu na ya wanyama,
12 wakampelekea Mose na Eleazari, na jumuiya yote ya Waisraeli iliyokuwa kambini katika nchi tambarare za Moabu, ngambo ya Yordani karibu na Yeriko.
13 Mose, kuhani Eleazari, na viongozi wote wa jumuiya ya Waisraeli walitoka kambini, wakaenda kuwalaki wanajeshi.
14 Mose alikasirishwa na maofisa wa jeshi na makamanda waliosimamia makundi ya majeshi 1,000 na makundi ya wanajeshi mamia waliorudi kutoka vitani.
15 Mose akawauliza, “Kwa nini mmewaacha wanawake hawa wote hai?