16 Eleazari mwana wa kuhani Aroni itampasa kuyatunza mafuta ya taa, ubani wa kunukia, tambiko za nafaka za kila siku, mafuta ya kupaka ili kuweka wakfu na kila kitu kilichowekwa wakfu katika hema hilo.”
17 Kisha Mwenyezi-Mungu akawaambia Mose na Aroni,
18 “Msiache ukoo wa familia za Kohathi miongoni mwa Walawi uangamizwe.
19 Basi, ili kuwaepusha wasije wakauawa kwa kuvikaribia vyombo hivyo vitakatifu sana utafanya hivi: Aroni na wanawe wataingia na kumpangia kila mmoja wao wajibu wake na kazi yake.
20 Lakini wazawa wa Kohathi hawataingia kamwe kuvitazama vitu hivyo vitakatifu sana; wakifanya hivyo watakufa.”
21 Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose,
22 “Wahesabu watu wa ukoo wa Gershoni, kufuatana na familia na koo zao;