33 Hii ndiyo itakayokuwa kazi ya wana wa ukoo wa Merari katika huduma yao yote ndani ya hema la mkutano, chini ya uongozi wa Ithamari mwana wa kuhani Aroni.”
34 Basi, Mose, Aroni na viongozi wa jumuiya yote wakafanya sensa ya watu wa ukoo wa Kohathi, kufuatana na familia zao,
35 wakawaorodhesha watu wote wenye umri kati ya miaka thelathini na hamsini, kila aliyefaa kuingia katika huduma ya hema la mkutano.
36 Idadi yao kufuatana na jamaa zao ilikuwa watu 2,750.
37 Hii ndiyo idadi ya watu wa jamaa ya Kohathi, ambao walihudumu katika hema la mkutano, ambao Mose na Aroni waliwahesabu kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.
38 Idadi ya watu wa ukoo wa Gershoni kufuatana na familia zao,
39 wenye umri kati ya miaka thelathini na hamsini, waliofaa kuhudumu katika hema la mkutano,